Serikali inaendelea kuwekeza katika elimu ya juu-Rais Dkt.Mwinyi

DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali ina wajibu mkubwa wa kuendelea juwekeza katika elimu ya juu ili kuzalisha wataalamu wengi zaidi watakaochangia maendeleo katika sekta tofauti na ustawi wa wananchi.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Kongamano la Kumuenzi Mkuu wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Tawi la Muhimbili (MUHAS) Rais wa Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi na Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Ndaki ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali inathamini Mafanikio Makubwa yaliofikiwa na Chuo cha Muhas tangu kuanzishwa kwake yanayochangia kuzalisha Wataalamu katika Sekta ya Elimu, Afya, Ufanyaji wa Tafiti na Utoaji wa huduma za Afya kwa jamii.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amekipongeza Chuo cha Muhas kwa Mradi wa Upanuzi wa Miundonbinu ya Chuo hicho kupitia Mradi Unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ushirikiano na Benki ya Dunia na kuishukuru kwa Misaada yake kwa Tanzania.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi amekipongeza Chuo cha Muhas kwa Kuandaa Kongamano Maalum la Kumuenzi Mkuu wa Kwanza wa Muhas Hayati Ali Hassan Mwinyi na Uamuzi wa Kuanzisha Mfuko Maalum wa Ali Hassan Mwinyi Endowment Trust Fund ikiwa ni njia ya kumuenzi.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amekishauri Chuo cha Muhas kuendeleza mambo mazuri yalioanzishwa na Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu ya chuo hicho alichokiongoza kwa miaka 17.
Rais Dkt.Mwinyi amezindua Vazi rasmi lililokuwa likivaliwa na Mzee Mwinyi wakati akihudumu akiwa Mkuu wa Chuo pamoja na kukabidhiwa Tuzo Maalum ya Kumuenzi kwa Utumishi wake Uliotukuka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news