Serikali ipo imara kusimamia haki,amani na mshikamano kwa wananchi-Shaka

MOROGORO-Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amesema,Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan haitaachaa wala kukengeuka kusimamia wajibu wake kwa wananchi na kuhakikisha haki, amani, mshikamano na utulivu wa kitaifa hauvurugwi kwa kiashiria chochote ovu, bila ustawi wa amani, vyombo vya kutoa maamuzi kutenda haki, utulivu na upendo.
Akizungumza leo Mkoani Morogoro wilayani Kilosa katika Kilele cha maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini,Shaka amesema hakutakuwa na njia mbadala ya kuwapatia wananchi maendeleo ya kisekta ikiwemo kuimarisha huduma za kijamii na tuamini kwamba jamii nayo haiko tayari kuishi kwa mashaka, hofu na wasiwasi.

Amesema watanzania ni waungwana hawataki na wala hawajazoe maisha ya mikiki mikiki na vishindo au matukio hatarishi,wanachokijua ni kuwaona viongozi wao wakisimamia amani, mshikamano, umoja wa kitaifa na upendo.

"Maisha ya mshikemshike na vurugu viko mbali na utamaduni wetu wa Kitanzania hivyo katika nyakati zote sera na mipango ya nchi imejikita katika suala la msingi la kuhubiri amani na utaifa kwa kujali utu, usawa na haki kwa kila binadamu bila kutazama dini, rangi au kabila.

"Tunayahimiza masuala hayo kwa kuwa bila ustawi wa umoja, amani na utulivu shime ya maendeleo itaporomoka,kabla ya Mungu hajashusha vitabu vyake vitukufu Zaburi,Taurat, Injili na Quraan yaaminika dunia yote iligubikwa na kiza cha dhulma lakini kutumwa kwa mitume yake ndipo mwanga wa haki ukaadhihirika na kupinga vitendo vyote ambavyo kwa kiasi kikubwa vilikandamiza misingi ya haki, usawa na utawala shariaa,"amesema.

Aidha, amesema ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi na vyombo vya kutoa Haki kuanzia ngazi za vijiji, uwajibikaji wa taasisi mbalimbali na muhimili wa mahakama ni muhimu kwa wananchi wa Kilosa.

"Serikali ya Wilaya ya Kilosa itasimamia mambo tisa mliyoshauri kufanyika katika kuboresha mfumo wa haki madai nchini ili kupunguza migogoro ikiwemo kuanzishwa kwa mabaraza vijijini yatakayosimamiwa na wazee wa mila ili kusuluhisha na kupunguza migogoro ya wananchi, Uwepo na utekelezaji wa sheria ndogo ndogo za halmashauri zinazosimamia matumizi bora ya ardhi,kuhamasisha usuluhishi wa migogoro kama njia mbadala ya
kutatua kesi kwa haraka na kwa gharama nafuu kabla na baada ya kufunguliwa mahakamani."

Pia amesema wananchi wanapaswa kushauriwa wawe na utamaduni wa kuwatumia wanasheria ili katika mashauri mahakamani au kwenye taasisi za usuluhishi ili kuepuka maswala ya kiufundi yanayoweza kuwakumba wakati wa uendeshaji wa mashauri yao,Kuboresha miundombinu na rasilimali za mahakama na taasisi za haki madai,Kuendelea kupambana na rushwa na kuongeza uwazi katika utoaji wa haki madai pamoja na Kuimarisha elimu ya sheria kwa wananchi ili wawe na uelewe haki zao,"alisema.

Hata hivyo amewaomba wanasheria na mawakili wa kujitegemea kuangalia upya ukubwa wa gharama huduma za sheria kuwa kubwa wakati mwingine wananchi wanyoge wanashindwa kuzitumia wakati wao ndio waathirika wakubwa migogoro.

Pia amehimiza ushirikiano kwa Taasisi za kusimamia haki madai zinapaswa kufuatilia migogoro kwa kushirikiana na serikali kuanzia ngazi zote kabla ya madhara kutokea na wakati mwingine kupelekea watu kupoteza maisha.

Sambamba na vyombo vya kusimamia haki vinapaswa kushughulikia kwa wakati malalamiko yanayofunguliwa kuondosha malalamiko ya wananchi ya kesi kuchukua muda mrefu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news