Serikali itaendelea kuwaunga mkono UWAWAZA-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea Kuunga mkono Harakati za Jumuiya ya Wawakilishi Wanawake (UWAWAZA) za kuwajengea uwezo wanawake katika maendeleo yao kisiasa,kiuchumi na kijamii.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Wajumbe wa Jumuiya hiyo waliofika Ikulu kujitambulisha na kumpongeza Dkt.Mwinyi.

Aidha Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,jumuiya hiyo ni sauti muhimu katika kupigania haki za Wanawake ndani na Nje ya Baraza la Wawakilishi na kuahidi kuendelea kuiunga Mkono kuyafikia malengo yao.
Ameeleza kufarijika na kazi zinazofanywa na Jumuiya hiyo za kuimarisha Ushiriki na kuongeza Idadi ya Wajumbe Wanawake katika Baraza la Wawakilishi kwani Uzoefu unaonesha Wanawake wanafanya Vizuri katika Uongozi.

Rais Dkt, Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwahamasisha Wanawake Kutosita kugombea nafasi za Uongozi katika Uchaguzi Ujao ili kuongeza Idadi yao katika Baraza la Wawakilishi.

Rais Dkt.Mwinyi ametoa ushauri kwa UWAWAZA kufanya tathmini ya Miaka 22 tangu Kuanzishwa kwake ili kubaini maeneo muhimu yanayohitaji Msukumo wa Serikali kuwainua Wanawake, kisiasa,kiuchumi na kijamii.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wawakilishi Wanawake Saada Mkuya Salum amempongeza Dkt, Mwinyi kwa Mafanikio ya Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara, Masoko , Hospitali na Vituo vya Afya ambavyo vimekuwa nyenzo muhimu kwa Ustawi wa Wanawake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news