Serikali na TFF kushirikiana kuhamasisha Elimu ya Mlipakodi

NA BENNY MWAIPAJA

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya majadiliano na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi, kuhusu maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta ya michezo hususan mpira wa miguu nchini, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akiongoza kikao wakati alipokutana na kufanya majadiliano na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi (kulia)kuhusu maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta ya michezo hususan mpira wa miguu nchini, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw.Yusuph Mwenda, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF, Bw. Wallace Karia, viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi zinazosimamia michezo nchini.

Katika majadiliano hayo, Serikali imeipongeza TFF na Bodi yake ya Ligi, kwa kusimamia kwa weledi masuala ya maendeleo ya soka na kuliletea Taifa heshima kubwa barani Afrika na kupewa jukumu la kuandaa mashindano ya CHAN na AFCON, na kukubaliana pia namna tasinia ya utamaduni, sanaa na michezo inavyoweza kutumika kuhamasisha uzalendo wa kulipa kodi kwa hiari, kupitia kampeni ya kudai na kutoa risiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF, Bw. Wallace Karia (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana na kufanya majadiliano kuhusu maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta ya michezo hususan mpira wa miguu nchini, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania-TFF, Bw. Wallace Karia, amekubali mapendekezo ya Serikali na kuahidi kuwa suala la ulipaji kodi ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa na kuahidi kuwa watalichukulia kwa uzito suala hilo katika michezo yote ya mpira wa miguu inayosimamia na Taasisi hiyo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi (watano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (wa nne kushoto), Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa nne kulia), Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw.Yusuph Mwenda (wa tatu kulia) na viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi zinazosimamia michezo nchini, baada ya kukutana na kufanya majadiliano kuhusu maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta ya michezo hususan mpira wa miguu nchini, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam).

Majadiliano hayo yaliwashirikisha viongozi wa juu wa Wizara ya Fedha, akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw.Yusuph Mwenda, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF, Bw. Wallace Karia, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Bw.. Almas Kasongo, viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi zinazosimamia michezo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news