Serikali yanunua magari 150 ya Zimamoto na kuyasambaza maeneo mbalimbali nchini

DODOMA-Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema kuwa Serikali inaendelea kuliimarisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kulipatia vitendea kazi ambapo sasa inatekeleza mradi wa ununuzi vifaa mbalimbali vya kuzima moto na uokoaji pamoja na magari 150 ya kuzima moto na uokoaji.
Bashungwa ameeleza hayo tarehe 03 Februari 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Shangai aliyetaka kujua Je, lini Serikali itanunua gari la Zimamoto Wilaya ya Ngorongoro.

“Kwa sasa Serikali inatekeleza mradi wa ununuzi vifaa mbalimbali vya kuzima moto na uokoaji pamoja na magari 150 ya kuzima moto na uokoaji,” amesema Bashungwa.

Amesema pindi magari 150 ya kuzima moto na uokoaji yatakapofika nchini, yatakayosambazwa nchi nzima ikiwemo Wilaya ya Ngorongoro.

Aidha, amesema Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeshaliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kununua magari 12 ya kisasa ambapo moja wapo lilitumiaka kuzima moto katika jengo gorofa la TRA Kariakoo.

Bashungwa amesema Serikali ipo mbioni kununua helikopta moja maalum kwa ajili ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambayo yataenda sambamba na kuwapatia Mafunzo Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news