DODOMA-Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inatekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi nchini inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira.
Ofisi imeingia makubaliano na vyuo 52 vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi ambavyo vimesajiliwa na mamlaka husika kutoa mafunzo katika fani mbalimbali;