Serikali yatoa angalizo mvua za masika Zanzibar

ZANZIBAR-Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Mhe. Hamza Hassan Juma ametoa tahadhari kwa wananchi dhidi ya mvua za masika zinazotarajiwa kunyesha nchini.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mwelekeo wa mvua za masika zinazotarajiwa kunyesha nchini katika kipindi cha mwezi wa Machi hadi Mei katika Baraza la Wawakilishi Chukwani amesema, mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani.

Amesema kuwa, mvua hizo zinatarajiwa kuanza kunyesha wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi na kumalizika wiki ya mwishio ya mwezi wa Mei ambapo mvua hizo zinaweza kuambatana na vipindi vifupi vya mvua kubwa na kuleta madhara kwa wananchi.

Waziri huyo amewataka wananchi kuhama katika maeneo yenye kutuhama maji hususani mabondeni na njia za asili ya maji ili kuepukana na athari za maafa na maradhi ya mlipuko.

‘’Mara nyingi mvua kubwa zinaambatana na upepo mkali, hivyo watumiaji wa bahari tunatakiwa kuchukua tahadhari zote kufutilia mueleko wa hali ya hewa kabla hatujafanya kuedelea na shughuli zetu za kawaida."

Aidha,Waziri Hamza alifahamisha kuwa kwa msimu huu wa mvua za masika kuna uwezekano wa kutokea uharibifu mkubwa wa barabara na kukatika au kuanguka kwa nguzo za umeme na hata kubomoka kwa madaraja hivyo amewasisistiza wananchi kuepuka kukaa katika maeneo hatarishi ili kuepukana na maafa.

Hata hivyo Waziri huyo amesema, Serikali imechukua juhudi kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya mitaro ya kupitishia maji ili kupunguza uharibifu wa baadhi ya maeneo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Zanzibar, Masoud Makame Faki amesema kuwa, mvua kubwa zinazoratajiwa kunyesha zina wastani wa milimita 850 ambazo zinaweza kuwa chini au juu ya hapo.

Akizungumzia kuhusiana na jua la utosini amesema, kiwango cha joto kwa mwaka huu kimeongeza ukilinganisha miaka 30 iliyopita wastani wa joto lililopo sasa ni wastani wa nyuzi joto 34.5 na nyuzi joto 35 kutokana na kuwa mwezi wa Febuari inakuwa ni kipindi cha kiangazi kinachosababisha kuongezeka kwa joto nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news