DAR-Serikali imeagiza Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na Benki ya TCB kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika soko la mitaji kwani ni muhimu kuongeza ushiriki wa wananchi katika uwekezaji wa hisa, ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia sekta binafsi kupata mtaji wa muda mrefu kwa njia endelevu.
Kauli hii ilitolewa na Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, wakati akizindua huduma ya uwekezaji wa hisa kupitia Popote Mobile App na kuiagiza Benki ya TCB kuhakikisha huduma hii inakuwa rahisi.
Pia,salama na inapatikana kwa wananchi wote bila vikwazo vya kiufundi na kuwa DSE na benki zishirikiane kupunguza gharama za uwekezaji na kuongeza ufanisi wa miamala ya hisa.

Ni kwa kutumia mifumo ya kidijitali kwani Serikali inalenga kuimarisha ushiriki wa wananchi katika masoko ya mitaji na kuchochea maendeleo ya uchumi wa soko huria nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TCB, Adam Mihayo, ameeleza kuwa uzinduzi wa Popote Mobile App ni hatua muhimu katika kuimarisha ujumuishaji wa kifedha na kuleta mageuzi katika soko la mitaji nchini.
Mihayo ameongeza kuwa, kuunganisha mifumo ya benki na DSE ni kunapanua wigo wa uwekezaji kwa kurahisisha upatikanaji wa hisa kwa wawekezaji wa rika zote, huku ikiongeza ukwasi katika soko la hisa na kuvutia wawekezaji wapya
Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Peter Nalitolela, amesema kuwa teknolojia hii inarahisisha ununuzi na uuzaji wa hisa moja kwa moja kupitia simu za mkononi bila kulazimika kutembelea madalali wa hisa au ofisi za soko.
Amesema, jambo hilo linapaanua wigo wa ushiriki wa wananchi katika soko la mitaji na kusaidia kampuni zinazoorodheshwa kupata mtaji.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMA), Nicodemus Mkama amepongeza uzinduzi wa Popote Mobile App.
Mkama amesema kuwa, ni hatua muhimu katika kuhakikisha Watanzania wanapata urahisi wa kuwekeza kupitia teknolojia ya kidijitali.
"Kwani teknolojia hii inawawezesha kufanya miamala ya hisa kwa njia salama na rahisi, bila vikwazo vya kifedha au kijiografia."

"Popote Mobile App ni suluhisho la kisasa ambalo linaruhusu Watanzania kufanya miamala ya hisa kupitia simu zao za mkononi, hali inayochochea ukuaji wa uchumi na kupanua fursa za uwekezaji katika masoko ya mitaji."
Tags
Benki ya Biashara Tanzania (TCB)
DSE Tanzania
Habari
Lipa Popote na TCB
Ofisi ya Msajili wa Hazina