Serikali yatoa taarifa muhimu kuhusu uendelezaji wa Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo

DODOMA-Serikali imesema kuwa,ipo katika hatua mbalimbali za kutekeleza Programu ya Ujenzi wa Eneo Maalumu la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ) ikiwa ni moja ya miradi 17 ya kielelezo iliyopo katika Mpango wa Tatu wa Miaka Mitano 2021/22-2025/2026.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 14,2025 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof, Kitila Mkumbo (Mb).

Waziri Prof.Mkumbo ameeleza kuwa, pamoja na uwepo wa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi walioonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), mazungumzo bado yanaendelea na hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa.

BSEZ ni sehemu ya miradi 17 ya kimkakati inayotekelezwa chini ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26) kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.

Mradi huu wa kimkakati unajumuisha ujenzi wa bandari ya kisasa, kongani za viwanda, kongani za TEHAMA, ukanda huru wa biashara na kituo cha reli. Serikali inashirikiana na sekta binafsi kupitia mpango wa ubia wa PPP (Public-Private Partnership) ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi unafanyika kwa ufanisi na kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

“Serikali inashirikiana na sekta binafsi kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi na uwazi,” ameongeza Waziri Mkumbo.

Serikali imesisitiza kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa mradi wa BSEZ, umma utaendelea kupatiwa taarifa rasmi kwa kila hatua muhimu ya maendeleo yake. Wananchi wametakiwa kupuuza taarifa zisizo rasmi na kufuatilia vyanzo sahihi vya habari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news