Serikali yatoa ufafanuzi asilimia 20 ya Kodi ya Ardhi

NA JOSEPHINE MAJURA
WF Dodoma 

SERIKALI imesema kuwa asilimia 20 ya mapato ya kodi zitarejeshwa katika halmashauri husika baada ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhusu kuboresha usimamizi na ukusanyaji wa kodi hiyo utakapo kamilika.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Seleman Mtenga wakati ambao Serikali itarejesha makusanyo ya Kodi ya Ardhi ya asilimia 20 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema Serikali kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2023/24 ilifanya marekebisho ya Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura 290 kwa kuzitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuingia Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) katika usimamizi na ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi na kuweka utaratibu wa urejeshaji wa asilimia 20 ya mapato kwa halmashauri ili kuziwezesha katika ufuatiliaji na ukusanyaji wa mapato hayo.
Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha wakifuatilia shughuli za Bunge jijini Dodoma. Kutoka juu ni Kamisha wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. Chotto Sendo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Daniel Masolwa.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF-Dodoma).

"Serikali iliweka utaratibu huo ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa kuna tija katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na pango la ardhi inaongezeka na kuondoa kero zilizokuwa zinawakabili walipa kodi kwenye maeneo husika,"alibanisha Dkt. Nchemba.

Alilihakikishia Bunge kuwa Mkataba huo utakapokamilika na kuwasilishwa Wizara ya Fedha, fedha hizo zitarejeshwa kama utaratibu unavyotaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news