IRINGA-Naibu Waziri wa Afya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, amesema serikali itatoa sh. milioni 600 kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha kisasa katika Kata ya Ukumbi, Wilaya ya Kilolo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange akizungumza na wananchi wa kata ya ukumbi (hawapo pichani) mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya kata ya ukumbi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za afya na elimu wilayani Kilolo.
Dkt. Dugange ametoa kauli hiyo alipokutana na wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya sekta ya afya na elimu wilayani humo.
Amepongeza juhudi za wananchi kwa kutenga ekari 13 za ardhi na kuchangia sh.milioni 45 kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitaboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa zaidi ya wakazi 14,000.
Wananchi wa kata ya ukumbi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao, mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya ukumbi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za afya na elimu wilayani Kilolo.
Mwonekano wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) linaloendelea kukamilishwa katika kituo cha afya cha kata ya Ukumbi kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Justin Nyamoga, mara baada ya kuwasili wilayani Kilolo kwa ajili ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za afya na elimu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuzungumza na wananchi wa kata ya ukumbi (hawapo pichani) mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya kata ya ukumbi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za afya na elimu wilayani Kilolo.
Baadhi ya wananchi wa kata ya ukumbi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Justin Nyamoga mara baada ya Mhe. Dugange kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya ukumbi, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za afya na elimu wilayani Kilolo.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Justin Nyamoga akizungumza na wananchi wa kata ya ukumbi (hawapo pichani) mara baada ya Mhe. Dugange kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya ukumbi, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za afya na elimu wilayani Kilolo.
"Serikali italeta si chini ya milioni 600 ili kukamilisha kituo cha afya cha kisasa chenye majengo yote muhimu, TAMISEMI tunataka ujenzi ukamilike na huduma za awali zianze kutolewa kwa wananchi ifikapo Machi 30, 2025,"amesema.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Mhe. Justin Nyamoga, amesema wananchi walijitoa kujenga kituo hicho baada ya zahanati waliyoitegemea kuwekwa kwenye eneo la barabara na kutarajiwa kubomolewa.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Dkt. Clemance Konkamkula, ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka 2011 kwa mapato ya ndani ya halmashauri, ambapo jengo la wagonjwa wa nje (OPD) limefikia asilimia 75 kwa gharama ya sh. milioni 132.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Dkt. Clemence Konkamkula akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Ukumbi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange (hayupo pichani) mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya kata ya ukumbi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za afya na elimu wilayani Kilolo.Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange akiwa katika ukaguzi wa jengo la nje la wagongwa (OPD) katika kituo cha afya kata ya ukumbi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za afya na elimu wilayani Kilolo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Bi. Siwema Jumaa akizungumza na wananchi wa kata ya ukumbi (hawapo pichani) mara baada ya Mhe. Dugange kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya ukumbi, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za afya na elimu wilayani Kilolo.
Halmashauri inahitaji sh. milioni 850 kukamilisha mradi, ikiwemo ujenzi wa wodi mbili, jengo la maabara, jengo la upasuaji, nyumba za watumishi, jengo la mionzi, na majengo mengine muhimu kwa utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa Kata ya Ukumbi.