Simamieni miradi kikamilifu na kwa ubora-Mhandisi Mativila

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Sekta ya Miundombinu katika Sekretarieti za Mikoa kusimamia miradi kikamilifu kwa mujibu wa mikataba ili kuhakikisha zinakuwa na ubora.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila akisisitiza jambo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa wakati wa kikao kazi chake na viongozi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.

Mhandisi Mativila ametoa maelekezo hayo leo Februari 5, 2025 kwenye kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma, kilicholenga kujadili utekelezaji wa miradi ya ujenzi, ukarabati, na matengenezo ya miundombinu katika Mikoa 26, Wilaya 139, na Halmashauri 184 nchini.

"Ubora wa kazi ni jambo la msingi. Kama ni jengo, lijengwe kwa viwango vinavyostahili. Kuna baadhi ya majengo yanapotembelewa na waheshimiwa wabunge, hubainika kuwa hayana ubora," amesisitiza Mhandisi Mativila.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila akizungumza na Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na viongozi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miundombinu, Eng. Gilbert Mwoga akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila kufungua kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.

Aidha, amewataka viongozi hao kuwa na mipango thabiti ya muda mfupi, muda wa kati, na muda mrefu ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, kama ilivyokusudiwa na serikali.

Mhandisi Mativila amewasihi kuboresha utendaji wao kwa lengo la kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watanzania wa mijini na vijijini.
Msanifu Majengo Bw. Jonafrey Mwagabagu wa Idara ya Miundombinu OR-TAMISEMI akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miundombinu, Eng. Gilbert Mwoga (kushoto) wakiwa katika kikao kazi na Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Msanifu Majengo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Chabu Nghoma akiahidi kusimamia utekelezaji wa miradi, mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila kufungua kikao kazi chao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Msanifu Majengo Bw. Jonafrey Mwagabagu wa Idara ya Miundombinu OR-TAMISEMI akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila akiwa katika kikao kazi na Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mororogoro Mhandisi Ezron Kilamhama akieleza namna watakavyosimamia utekelezaji wa miradi, mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila kufungua kikao kazi chao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.

Naye, Katibu Tawala Msaidizi wa Miundombinu wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Ezron Kilamhama, ameahidi kushirikiana na wahandisi wa halmashauri kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa mujibu wa mikataba na kwa viwango vinavyostahili.

Msanifu Majengo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Chabu Nghoma, amesema wataandaa mpango kazi wa utekelezaji wa miradi kwa ufanisi na kuuwasilisha kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI ndani ya mwezi wa pili kwa ajili ya tathmini.

Ofisi ya Rais – TAMISEMI ina jukumu la kuratibu matengenezo, ukarabati, na ujenzi wa miundombinu ya barabara, majengo, na miundombinu mingine katika ngazi za mikoa, wilaya, na mamlaka za serikali za mitaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news