Simba SC hesabu kali Ubingwa wa Ligi Kuu, yaichapa Namungo FC mabao 3-0

LINDI-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Ushindi huo, unaifanya Simba SC kuvunja mwiko katika Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi kutokana na kutopata alama tatu katika miaka miwili mfululizo iliyopita.

Katika mtanange huo wa Februari 19,2025 mlinzi wa kati wa Namungo Derick Mukombozi alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 35 baada ya kucheza mchezo usio wa kiungwana.

Jean Charles Ahoua aliwapatia Simba SC bao la kwanza dakika ya 49 kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti baada ya mlinzi Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Leonel Ateba alikosa mkwaju wa penati uliookolewa na mlinda mlango Jonathan Nahimana dakika ya 51 baada ya Elie Mpanzu kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na Hassan Kibailo.

Ahoua aliwapatia bao la pili dakika ya 72 kwa mkwaju wa penati baada ya Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na Anthony Mlingo.
Steven Mukwala aliwapatia bao la tatu dakika ya 92 baada ya shuti kali lililopigwa na Valentine Nouma kumgonga mlinzi wa Namungo kabla ya kumkuta mfungaji.

Ushindi huo unaifanya Simba SC kufikisha alama 50 wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 19 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news