Simba SC ina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu-Fadlu Davids

DAR-Kocha Mkuu wa Simba SC,Fadlu Davids amesema makosa mawili ya dakika ya mwanzo na ya mwisho yamewagharimu na kupelekea sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Azam FC licha yakuwa na mchezo bora uwanjani.
Ni kupitia mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao umepigwa Februari 24,2025 katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Fadlu amesema, bado wana nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu kwa kuwa tofauti ya alama iliyopo ni ndogo,hivyo wanapaswa kushinda kila mchezo ili kufikia malengo.

Kwa matokeo hayo Simba SC inaendelea kubakia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania ikiwa na alama 51 baada ya mechi 20.

Aidha, watani zao Yanga SC wanaendelea kutamba kileleni mwa ligi kwa alama 55 baada ya mechi 21.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news