MANYARA-Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC dhidi ya Fountain Gate FC uliopigwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.
Mchezo huo wa Februari 6,2025 ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini, Simba SC walifika zaidi langoni kwa Fountain Gate.
Dakika 15 kabla ya kuelekea mapumziko waliongeza mashambulizi langoni mwa Fountain Gate, lakini kikwazo kilikuwa mlinda mlango John Noble.
Leonel Ateba awatupatia Simba SC bao la kwanza dakika ya 57 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ladaki Chasambi.
Fountain Gate walisawazisha bao hilo dakika ya 75 baada ya Chasambi kujifunga wakati aliporudisha mpira mrefu uliomshinda mlinda mlango Moussa Camara.
Mlinda mlango John Noble alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya pili ya nyongeza baada ya kupoteza muda.
Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Februari 6,2025;