DAR-Klabu ya soka ya Simba SC, imetozwa faini ya shilingi milioni moja kwa kosa la walinzi wake kuwazuia walinzi wa uwanjani (stewards) kumkamata shabiki aliyekuwa akitaka kuingia uwanjani baada ya mchezo wao dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa Desemba 28, 2024.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) pia imeeleza Kocha wa Fountain Gate FC, Robert Matano ametozwa faini ya shilingi laki tano kwa kosa la kuwashutumu waamuzi waliochezesha mechi yao dhidi ya Simba SC iliyopigwa Februari 6, 2025.