SINGIDA-Uongozi wa Singida Black Stars umeeleza kushutushwa na taarifa za kocha wao,Hamdi Miloud raia wa Algeria kutangazwa kuwa ni Kocha Mkuu wa Young Africans Sports Club.
Yanga SC ilimtangaza kocha huyo mwenye uraia wa Algeria na Ufaransa kuwa kocha wake mpya akichukua mikoba ya Sead Ramovic ambaye ameondoka klabuni hapo baada ya kuvunja naye mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili.