MOROGORO-Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kimeanza kuuza mbegu bora za malisho ya mifugo ambapo kupitia Kitengo cha Nyanda za Malisho kimewakaribisha wafugaji kuchangamkia fursa hiyo.
Bw. Winfred Ngilangwa kutoka Idara ya Shamba la Mafunzo SUA ameeleza hayo Februari 6, 2025 wakati wakivuna mbegu za malisho zilizonunuliwa na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ya mkoani Arusha ambapo ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wafugaji binafsi kufika chuoni kununua hizo mbegu.
Bw. Ngilangwa amesema mpaka sasa SUA imeuza kilo 8000 ambazo ni sawa na tani 8 za nyasi aina ya Juncao ambazo hutumia miezi mitatu kukua tangia kupandwa kwake.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiG7WYM-J4WkW3__a-jgoalenXVlVeZKozEVUAMpZ_RumM0AHj3J7NRA_kxIOEuDwUzwwTf4ZfUKQOTAWItpR2fiquNodC0H7JavrFC3ZbvR2k79Da7N5HgD1GJygR5WSHgzWR599jbjuMZyG3CN1kmWilGcpVXYhwbzkllmNFMFvapaBstKEVZB59DeiyK/s16000/1001179466.jpg)
Kwa upande wake, Bw. Yeremia Ntandu akizungumzia mwitikio wa wafugaji kununua mbegu za nyasi amesema kumekuwa na mwitikio mzuri ambapo wafugaji wamekuwa wakinunua kila mmoja kwa mahitaji yake huku akibainisha kuwa ukuzaji wa hizo nyasi ni rahisi kwani hauna gharama kubwa.