Suleiman Mwalimu asajiliwa Wydad AC nchini Morocco
MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars, Suleiman Mwalimu (25) ambaye alikuwa anaitumikia klabu ya Fountain Gate FC kwa mkopo, amejiunga na Klabu ya Wydad AC ya nchini Morocco kwa mkataba wa miaka minne.
Suleiman Mwalimu anakuwa chaguo la pili baada ya klabu hiyo kumkosa Clement Mzize wa Young Africans Sports Club (Yanga SC) kwenye dirisha hilo.