ADDIS ABABA-Februari 16,2025 katika siku ya pili ya muendelezo wa mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Wake wa Marais wa Afrika (OAFLAD) ukumbi wa Umoja wa Afrika , Addis Ababa, Ethiopia Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi amehutubia kikao cha Building on Beijing.

Mama Mariam Mwinyi ameelezea mafanikio katika elimu, afya, mageuzi ya sheria, uwezeshaji wa kiuchumi, na maamuzi nchini Tanzania na Zanzibar, miaka 30 tangu maazimio hayo.
Chini ya uongozi wake, Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) inaendelea kutekeleza ahadi za Tamko la Beijing, ikiwawezesha wakulima wa mwani 1,690+, kwa lengo la kufikia 5,000 ifikapo 2030. Katika afya ya uzazi, wasichana 8,600 mashuleni wamenufaika na taula za kufua, kupunguza uhaba wa taulo za hedhi na utoro shuleni.
Halikadhalika Kampeni ya Afya Bora Maisha Bora imefikia wanufaika 17,200+, ikilenga utapiamlo, vifo vya akina mama, na magonjwa yasiyoambukiza (NCDs).
Vilevile, ameeleza kuwa mfumo wa Usimamizi wa Kesi za GBV Zanzibar unaleta mabadiliko makubwa katika ufuatiliaji na usimamizi wa kesi za ukatili wa kijinsia.
Kwa upande mwingine Mama Mariam Mwinyi anaendelea kujitoa kuimarisha uongozi wa wanawake, kulinda urithi wa kiafrika, na kusukuma mbele maendeleo endelevu.
Tags
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Habari
Kimataifa
Mama Mariam Mwinyi
Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)
Zanzibar News