NJOMBE-Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Njombe Noel Mseo, alihabarisha umma kupitia vyombo vya habari na kueleza kuwa katika Mkoa wa Njombe wamefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 32 ya thamani ya shilingi bilioni 15.8 katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba, 2024.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TAKUKURU Njombe Februari 7,2025 ambapo kati yake, miradi tisa yenye thamani ya shilingi Bilioni 13.1 ilionekana kuwa na kasoro ndogondogo na ushauri ukatolewa ili kurekebisha kasoro hizo.
Mkuu huyo alieleza kuwa, katika kuhakikisha ubora wa miradi hiyo, Kamati za Ujenzi zinazosimamia utekelezaji wa miradi zilipewa elimu ya namna ya kutekeleza miradi hiyo na kudhibiti ubadharifù unaoweza kutokea katika utekelezaji wa miradi.