KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa mamlaka aliyopewa Kwa mujibu wa kifungu cha 14 (4) cha Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sura ya 427, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 5(1) ya kanuni za Utumishi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji za mwaka 2008 anatangaza nafasi za ajira ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa vijana wenye sifa zifuatazo:-
1.Wenye elimu ya kidato cha Nne
Sifa za mwombaji.
a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
b) Awe na cheti cha kuzaliwa
c) Awe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Utambulisho iliyotolewana Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA)
d) Awe na afya njema kimwili na kiakilie) Asiwe na Kumbukumbu za Uhalifu
f) Awe hajaoa au kuolewa
g) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (Tatoos)
h) Awe hajawahi kutumia aina yoyote ya madawa ya kulevya
i) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya Zimamoto na Uokoaji
j) Awe hajawahi kuajiriwa serikalini
k) Awe mwenye urefu usiopungua futi 5.7 kwa mwanaume na futi 5.4 kwa mwanamke
I) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa
m) Umri kuanzia miaka 18 hadi 25
Tags
Ajira Jeshi la Polisi Tanzania
Ajira Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Fursa za Ajira
Fursa za Ajira Tanzania
Habari
Said kassim chegeka
ReplyDelete