Tanzania kinara Afrika uunganishaji Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) na Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE)

PETER HAULE NA
ASIA SINGANO

TANZANIA imefanikiwa kuwa nchi ya kwanza kuunganisha Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) na Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) kwa nchi za Afrika uliotambuliwa na Jumuiya ya Madola na kuifanya kuwa kitovu cha mafunzo ya Mifumo hiyo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (mbele) akiongoza mjadala wakati wa mafunzo kuhusu Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) na Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) iliyounganishwa, kwa Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, yaliyofanyika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Dodoma.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, alipokuwa akifungua mafunzo kwa Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya waliokuja nchini kujifunza namna Mifumo hiyo inavyofanya kazi.

Alisema kuwa Timu hiyo ya Wataalam imekuja ili kujadiliana na kujifunza katika maeneo ya Mifumo ya kuweka takwimu za masuala ya madeni kwa kuwa nchi hizo pia zinakopa kutoka kwa wadau mbalimbali, hivyo kutakiwa kuweka takwimu za ukopaji vizuri na kulipa madeni kwa wakati.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya akifungua mafunzo kuhusu Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) na Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) iliyounganishwa, kwa Timu ya wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, yaliyofanyika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Dodoma.

“Tunashukuru tumewapokea wajumbe hawa na sisi tutajifunza kutoka kwao namna wanavyofanya kazi, tunaona kwamba ushirikiano huu utakwenda vizuri na nisehemu tu ya mambo mengi ambayo tumekuwa tukiyafanya kwa ushirikiano ili kuboresha utendaji na namna tunavyotoa huduma kwa watu wetu”, alisema Bw. Mwandumbya

Alisema kuwa Wizara ya Fedha itahakikisha mafunzo hayo yanaenda vizuri na malengo yaliyopangwa yanatimia ili nchi hizo ziweze kuboresha utendaji wake kwa upande wa kuweka takwimu sawasawa lakini pia kulipa madeni.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mifumo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Dkt. John Sausi, akitoa mafunzo kwa Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, ikiongozwa na Bw. Jeremiah Tomno, kuhusu Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) na Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) iliyounganishwa, jijini Dodoma.

Mafunzo hayo yanasaidia kuwa waangalifu kwa upande wa kukopa na kuzisaidia nchi hizo kuwa salama kiuchumi na kuepusha madeni yanayoweza kuziletea changamoto za maendeleo ya kiuchumi.

Kwa upande wake Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, Jeremiah Tomno, alisema kuwa malengo makubwa ya ziara yao yalikuwa kujifunza namna Tanzania ilivyo unganisha Mfumo wa Muse, CS- Meridian na Benki Kuu.

Alisema kuwa kutokana na mawasilisho yaliyofanyika, wamejifunza mambo mengi hata waliyokuwa hawajayatarajia ambayo ni mambo mema kwao, na kwamba watawasilisha mada ambazo zitakuwa na manufaa kwa pande hizo mbili.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya akiagana na Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, Jeremiah Tomno, baada ya kufungua mafunzo kuhusu Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) na Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) iliyounganishwa, kwa Timu ya wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, yaliyofanyika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Dodoma.

Bw. Tomno aliongeza kusema kuwa wanafanya hayo kwa kuwa nchi hizo zipo katika Jumuiya na Ukanda mmoja, hivyo wanahitaji kufanya mambo ambayo kwa kiasi kikubwa yanatakiwa yafanane kwa kuwa wawekezaji wanazitazama nchi hizo kwa namna inayofanana.

Alishukuru kwa niaba ya Timu yake kwa mapokezi na kwamba wamejipanga kuhakisha wanapata ujuzi wa kutosha na wanatoa pia ujuzi wao kwa manufaa ya pande hizo mbili.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya akiagana na Kamishna wa Idara ya Bajeti wa Wizara ya Fedha Kenya, Dkt. Margaret Nyakang’o, baada ya kufungua mafunzo kuhusu Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) na Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) iliyounganishwa, kwa Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, yaliyofanyika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Dodoma.

Naye Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mifumo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Dkt. John Sausi, alisema kuwa baada ya Serikali kufanikiwa kuunganisha Mfumo wa MUSE na Mfumo wa Usimamizi wa Madeni, Jumuiya ya Madola, waliona utekelezaji na usimamizi wa deni kwa Tanzania umekuwa mzuri, jambo lililosababisha nchi nyingi kuja kujifunza Tanzania.

“Wizara ya Fedha imekuwa ikitekeleza maelekezo ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu kuunganisha Mifumo ambayo imekuwa ikitumika, ambapo Wizara ya Fedha imefanikiwa kuunganisha Mifumo mingi hadi sasa tangu maelekezo hayo yalipotolewa.
Timu ya wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, ikiongozwa na Bw. Jeremiah Tomno, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo kuhusu Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) na Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) iliyounganishwa, jijini, Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Dodoma).

Alisema kuwa Wizara ya Fedha imeunganisha Mifumo kuanzia ukusanyaji wa mapato hadi namna mapato hayo yanavyotumika na hivyo kutokuwa na mwingiliano wa watu katika Mifumo hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news