Tanzania kuchangamkia fursa ya ufadhili wa masomo kutoka Umoja wa Ulaya

BUNDAPEST-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), katika mwendelezo wa ziara yake nchini Hungary, amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. György Hölvényi, Mbunge wa Bunge la Ulaya (EP) kutoka Hungary na Ripota wa Elimu wa Kamati ya Maendeleo ya Bunge la Umoja wa Ulaya.
Katika mazungumzo hayo, Waziri Kombo ameeleza uhitaji wa kuzitumia vyema fursa za kielimu kutoka Umoja wa Ulaya ambapo Mhe. Hölvényi alieleza kuhusu fursa ya ufadhili wa jumla ya Euro bilioni 8 kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa elimu hususan kwa watoto wenye mahitaji maalum barani Afrika.
Kwa kuzingatia ushirikiano mzuri baina Tanzania na Umoja wa Ulaya, Mhe. Hölvényi alisisitiza ni vyema Tanzania ikachangamkia fursa hiyo ili kuwa miongoni mwa nchi za kipaumbele zitakazonufaika na ufadhili huo.

Aidha, baadhi ya wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wamepanga kufanya ziara nchini Tanzania kuanzia tarehe 23 hadi 26 Februari, 2025 ili kuimarisha ushirikiano baina ya Bunge la Tanzania na Umoja wa Ulaya pamoja na kutembelea miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini hasa miradi ya elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news