BUDAPEST-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hungary zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya Ushirikiano katika eneo la Mafunzo ya Kidiplomasia.

MoU hiyo inalenga kubadilishana ujuzi na uzoefu pamoja na kubadilishana wanafunzi wa diplomasia ili kupata elimu itakayokidhi uhitaji wa sasa ambapo wadau wakuu ni Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim kwa upande wa Tanzania na Chuo cha Diplomasia cha Hungary.
Hati hiyo imesainiwa jijini Budapest, Hungary na Waziri wake Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Péter Szijjártó.