ADDIS ABABA-Tanzania kupitia TAKUKURU, imeibuka mshidi katika mchakato wa kugombea naafasi ya Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika (AUABC) atakayewakilisha Ukanda wa Afrika Mashariki.
Uchaguzi huo wa wajumbe umefanyika Februari 13, 2025 Addis AAbaba nchini Ethiopia, ukijumuisha wagombea wawili kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki ambao ni Nchi ya Madagascar na Tanzania.
Mjumbe anayetoka TAKUKURU Bw. Benjamin Kapera (pichani), ameshinda kwa kupata kura 33 kati ya 48 zilizopigwa (Sawa na asilimia 69), ambapo Mgombea kutoka Madagascar (aliyekuwa akitetea uwakilishi kwa awamu ya pili) akipata kura 14.
Bodi hii ina jukumu la kushauri na kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa mwaka 2003 (AU Convention on Preventing and Combating Corruption) ambao Tanzania imeusaini na kuridhia utekelezaji wake.