TEITI kuzindua Ripoti ya 15 ya Uzinduaji,yatoa elimu kwa watu wenye uono hafifu

DODOMA-Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) imepanga kuweka wazi ripoti ya 15 ya TEITI kabla ya Juni mwaka huu.
Hayo yameelezwa leo Februari 20, 2025 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI, Ludovick Utouh kupitia hotuba iliyosomwa na Kaimu Meneja Kitengo cha Uwazi na Uwajibikaji ya TEITI, Erick Ketagory wakati wa kuzindua semina maalumu ya kuhamasisha matumizi ya takwimu za ripoti za TEITI kwa wanachama wa Chama cha Wasioona waliotoka wilaya zote za Mkoa wa Dodoma.

Alisema mpaka sasa TEITI imesatoa ripoti 14 na kwa sasa ipo katika maandalizi ya ripoti ya 15 kwa kipindi cha Julai 1, 2022 hadi Juni 30, 2023 na itawekwa wazi kabla ya Juni mwaka huu.
TEITI hutakiwa kuweka wazi malipo ya kodi na mapato yaliyofanywa na kampuni za madini, mafuta na gesi asilia kwa Serikali kila mwaka.

Hadi sasa Tanzania imechapisha na kutoa ripoti 14 kwa kipindi cha Julai 1, 2008 hadi Juni 30, 2022 zinazolinganisha malipo yaliyofanywa na kampuni za madini, mafuta na gesi asili na mapato yaliyopokelewa na Serikali.

Ripoti ya 14 ya TEITI ambayo hutolewa katika kutimiza matakwa ya Kimataifa ya Uwazi na Uwajibikaji (EITI) ilionesha kuwa sekta ya madini ilichangia asilimia 80.21 ya Mapato yote ya Serikali yatokanayo na rasilimali madini, mafuta na gesi asilia kwa mwaka 2021/22.

Aidha, Getagory alisema pia TEITI imekuwa ikiandaa na kuchapisha kwa waandishi maalum ya nukta nundu ili kuwafikia kundi la wananchi wasioona hapa nchini, mtakumbuka kuwa rasilimali madini, mafuta na gesi asili ni za wananchi wote.

“Hivyo TEITI imeona ni vyema kuandaa ripoti zetu kwa nukta nundu ili wananchi wote wapate fursa ya kuelewa na kufahamu juu ya taarifa na takwimu mbalimbali katika sekta ya madini, mafuta na gesi asilia ili waweze kuhoji manufaa ya rasilimali hizo kwa nchi na wananchi.”

Akisoma hotuba ya Katibu Mtendaji wa TEITI, Mariam Mgaya, Kaimu mkuu wa kitengo cha Tehama na Takwimu TEITI, Bakari Birika alisema katika warsha hiyo washiriki watapata fursa ya kupata uelewa kuhusu majukumu ya TEITI na namna ya kutumia takwimunzinazoandaliwa kupitia Ripoti za TEITI.“Taasisi inajukumu la kujenga mfumo wa uaandaji wa Ripoti za TEITI na kuwajengea uwezo wananchi katika kutumia Takwimu zinazotokana na taarifa za TEITI kupitia warsha mbalimbali na ndio maana tumeandaa warsha hii kwa kundi hili ili nao wawe na mchango wa kuchangia katika sekta hizi.”
Aidha, Birika alisema mpango wa TEITI pia imepanga kuweka wazi mikataba ambayo serikali imeingia na kampuni za madini, mafuta na gesi na kujenga rejista ya wamiliki wa kampuni za madini, mafuta na gesi asilia.

Naye Mwenyekiti Chama cha Wasioona Mkoa wa Dodoma, Omari Lubuva alishukuru kwa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia wao kupata uelewa kuhusu TEITI na kujua fursa zilizopo.

“Makundi ya walemavu hususani wasio ona wamekuwa wakisahaulika katika mambo mengi, hivyo tunaishukuru TEITI kwa kuona umuhimu wa sisi kupata elimu na uelewea na kutambua fursa zilizopo na kuzitumian kama ilivyo kwa watanzania wengine.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news