DAR-Timu ya Taifa ya ngumi kwa upande wa wanawake leo imeingia kambini rasmi kwaajili ya kujiandaa na mashindano ya ubingwa wa Dunia.
Mashindano hayo yatafanyika nchini Serbia mwezi Machi mwaka huu ambapo Tanzania imepata nafasi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa Duniani kwa upande wa mchezo wa ngumi.
Kambi hiyo iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam itatumika kwaajili ya maandalizi ya mabondia hao ambapo watakaa hapo kwa takribani siku ishirini na kambi itavunja Machi tatu mwaka huu na siku inayofuata baada ya hapo itakua ni kwaajili ya safari ya kuelekea nchini Serbia.