DAR-Timu ya Taifa ya ngumi kwa upande wa wanawake imeeendelea na mazoezi huku bado ikiwa kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya ubingwa wa Dunia.
Mashindano hayo yatafanyika nchini Serbia mwezi Machi mwaka huu ambapo Tanzania imepata nafasi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa duniani kwa upande wa mchezo wa ngumi.
Kambi hiyo iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam ni mahususi kwa timu hiyo ya Taifa kwaajili ya maandalizi ya mabondia hao ambapo watakaa hapo kwa takribani siku ishirini na kambi itavunja Machi tatu mwaka huu na siku inayofuata baada ya hapo itakua ni kwaajili ya safari ya kuelekea nchini Serbia.
Kufanikiwa kushiriki kwa mashindano hayo italeta tija kwa maendeleo ya michezo Tanzania na kwa mabondia wanawake watakaoshiriki kwani kuna uwezekano wa kujikomboa kiuchumi hasa kutokana na zawadi watakazopata washindi wa mashindano hayo kwa jumla ya dola za kimarekani 2.88 milioni zilizoandaliwa kwa ujumla kwa mgawanyo kama ifuatavyo.
Medali ya dhahabu zawadi yake ni dola za kimarekani 100, 000 sawa na milioni 255 za kitanzania.
Medali ya fedha zawadi yake ni dola za kimarekani 50,000 sawa na milioni 126. 9na laki tano za kitanzania.
Medali ya shaba zawadi yakeni dola za kimarekani 25,000 sawa na milioni 63. 5 za kitanzania.
Tano bora zawadi yake dola za kimarekani 10,000 sawa na milioni 25. 4 za kitanzania.