Tuendelee kuiombea nchi amani kuelekea Uchaguzi Mkuu-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, jamii ina wàjibu wa kujifunza umuhimu wa amani kupitia mambo yanayojiri katika nchi zilizokosa amani ulimwenguni.
Akizungumza katika Dua Maalum ya Kuiombea Nchi pamoja na Viongozi Wakuu, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan iliyofanyika Chaani Tangini, Alhaj Dkt.Mwinyi amesema,amani ni jambo la kwanza kwa Taifa lolote linalohitaji Maendeleo na Maisha Bora ya Watu wake.
Amesema kuwa,watu wanaohitaji maendeleo na kuwepo kwa haki wanapaswa kufahamu kuwa amani ya nchi ndio jambo la kwanza linalohitaji kupewa kipaumbele.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameendelea kuwahimiza wanasiasa,waandishi wa habari na viongozi wa dini kutumia nafasi zao kuhubiri umuhimu wa amani.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewasisitiza wananchi kuendelea kuiombea nchi amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba na kuwashukuru walioandaa dua hiyo aliyoielezea kuwa ni zawadi kubwa kwa mwanadamu.
Baada ya Dua hiyo Rais Dkt. Mwinyi alisalisha waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Adhuhuri Kiwanjani hapo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news