ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezisisitiza jumuiya za Chama Cha Mapinduzi kuwahamasisha wanachama na wananchi kujiandikisha na kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili CCM ishinde kwa kishindo.
Dkt. Mwinyi ambaye ni Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM ameyasema hayo alipozungumza na wanachama na wananchi Mauwani, Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba katika Mkutano Maalum wa Mapokezi yake baada ya kuteuliwa hivi karibuni kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar.