DODOMA-Tume ya TEHAMA, imeelezea kufurahishwa na uamuzi wa Serikali wa kuanzisha Maonesho ya Anuani za Makazi ikisema ni jukwaa muhimu la kufikisha elimu juu ya mchango wa anuani katika uchumi wa kidigitali.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4c41HS_8IsDTGaCQ14v-hxqHK4PrM-jCje0yMux28pgRKnshm_AiyEXL4upNXQcxXVi1DqD6Yxwc8XsvWB8s1NkP71yZb9LAvvB9FEwaHAPLCDU2qolukVFkZDHD93b5sIHBz4mpeuwrVCgAQU21N7vW0-wTqGsFF2jdGthnp0YM_QW2JfXOpvsRzc-So/s16000/1001174199.jpg)
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya Anuani ya Makazi, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga alisema Mfumo wa Anwani za Makazi ni nyenzo ya utambuzi ambayo inarahisisha utoaji na upokeaji wa huduma mbalimbali ili kuchochea maendeleo ya Kiuchumi na kijamii.
Alisema katika zama hizi ambazo Mapinduzi ya 4,5 na 6 ya viwanda yanategemea matumizi ya TEHAMA, ushiriki wa Tume ya Tehama katika kutoa elimu kwa Watanzania ni muhimu kwani wao ni sehemu ya kusaidia uwapo wa mifumo thabiti ya utambuzi.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa (Katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wizara na taasisi zinazoshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Anuani za Makazi yanayoendelea jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto waliosimama na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-YIhaf4eFy9C7ZrCeSNzcs8Ml25loW9Na_M30hZwjfmg0TSlYm9TjgstzZZHBn8Z4iaiqR6knIosiXcSo0VeZ39awyAr8cSIrVQIr-OXXOjwHLmHl8u-EoCufX00g1Hd5QzD787EB1us5e4GFtW40SptwGtLwgq9Uha9jB4oQIu3IB7a5qFN87Q8NUMng/s16000/1001174201.jpg)
“Katika maonesho haya, ni muhimu sana kwetu sisi kama Tume, lakini kwa taifa kwa ujumla kuweza kuendelea kuwafikia Watanzania wa mijini na vijijini waweze kufahamu umuhimu wa anuani za makazi kidigitali ili kila mmoja ashiriki katika kuujenga uchumi wa kidigitali.
“Kote duniani inafahamika kuwa uchumi wa kidigitali ni uchumi wa watu. Na ili watu waweze kutumia mifumo kufanya shughuli zao kidigitali, wanahitaji kupata uhakika wa kufikishiwa huduma katika maeneo yao, iwe ofisini na nyumbani. Kwa hiyo katika utambuzi wa kidigitali, anuani ni ya msingi sana,” alisema Dkt. Mwasaga huku akisisitiza wabunifu kuelekeza nguvu katika ubunifu ili kuwafikia Watanzania.
Maonesho hayo ya anuani za makazi yaliyozinduliwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa jijini Dodoma, yakiwa na kauli mbiu ya: “Tambua na Tumia Anwani ya Makazi Kurahisisha Utoaji na Upokeaji wa Huduma” yameshirikisha pia Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mbali ya Tume ya TEHAMA, taasisi nyingine zinazoshiriki sambamba na Ofisi ya Rais (TAMISEMI).