Tusipandishe bei za bidhaa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza wafanyabiashara kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kufanya biashara kwa uadilifu na kuwa na huruma kwa wananchi.Alhaj Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Masjid Jibril Mkunazini alipojumuika katika Sala ya Ijumaa.
Aidha,Alhaj Dkt.Mwinyi amesema kumekuwa na kawaida na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei bidhaa wakati huo.

Amefahamisha kuwa,Serikali imekuwa ikipunguza ushuru katika Mwezi wa Ramadhani, hivyo si jambo jema kwao kupandisha bei za bidhaa na kuwaongezea mzigo wananchi.
Akizungumzia suala la Uchaguzi Mkuu ujao Alhaj Dkt.Mwinyi amewasisitiza waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi kudumisha amani ili uchaguzi huo ufanyike kwa utulivu na amani.
Wakati huo huo Rais wa Zanzibar Alhaj Dkt.Mwinyi amefika Jamati la Jumuiya ya Ismailia Aga Khan Kiponda na Kusaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha kiongozi wa jumuiya hiyo Aga Khan wa Nne Prince Shah Karim Al- Husseini aliyefariki hivi karibuni Mjini Lisbon nchini Ureno akiwa na Miaka 88.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news