Tutaendelea kushirikiana na vyombo vya habari kote nchini-BoT

NA GODFREY NNKO

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kuwa, itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari kote nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kina kuhusu masuala ya uchumi na masoko ya fedha.
Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Vicky Msina akimkaribiusha mgeni rasmi kufungua semina hiyo leo Februari 25,2025 katika ofisi za tawi la BoT mkoani Mtwara.

Hayo yamebainishwa leo Februari 25, 2025 na Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mtwara, Nassor Omar wakati akifungua semina ya siku tatu kwa waandishi wa habari za uchumi kutoka mikoa mbalimbali kwa niaba ya Naibu Gavana, Julian Banzi Raphael.
Semina hiyo ambayo inaratibiwa na BoT inawajumuisha waandishi wa habari za uchumi kutoka Zanzibar, Ruvuma, Dar es Salaam, Mtwara na Lindi.

Katika semina hiyo ya siku tatu, wanahabari wanapata wasaa wa kujifunza kuhusu muundo na majukumu ya Benki Kuu,maana ya Sera ya Fedha inayotumia Riba ya Benki Kuu, umuhimu wa Benki Kuu kuwa na dhahabu kama sehemu ya akiba yake ya fedha za kigeni.

Mada nyingine ambazo watajifunza ni kuhusu umuhimu wa matumizi ya shilingi ya Tanzania katika shughuli za uchumi nchini,historia ya fedha za Tanzania, alama za usalama na utunzaji wa fedha hizo.

Pia, wanahabari watajifunza kuhusu mafanikio na chanagamoto za usimamizi wa sekta ya huduma ndogo za fedha, malipo ya kidigitali kwa bidhaa na huduma,utekelezaji wa kanuni za kumlinda mteja wa huduma za kibenki benki kuu duniani na fedha za kidijitali (CBDC).
Aidha,wanahabari watapata fursa ya kutoa mtazamo wao kuhusu Benki Kuu ya Tanzania (BoT), pia watajifunza kuhusu mfumo mpya wa utekelezaji wa Sera ya Fedha.

Amesema, semina hizi ni ishara kwamba Benki Kuu inatambua na kuthamini mchango wa vyombo vya habari katika kushiriki kufikisha taarifa mbalimbali za uchumi na masoko ya fedha ambazo zinagusa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Meneja Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Vicky Msina amesema kuwa,semina hizi ambazo ni jumuishi kwa wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini zimekuwa zikifanyika kwa takribani miaka 17 sasa.
Amesema kuwa,BoT kupitia Gavana Emmanuel Tutuba inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kupasha habari na kuelimisha umma kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo uchumi na masoko ya fedha, hivyo ushirikiano huo utaendelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news