Ujenzi ofisi mpya ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya kupangiwa bajeti 2025/26

DODOMA-Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuweka kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 maombi ya fedha kwaajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
Mhe. Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma leo Februari 14, 2025 kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Lupa, Mhe. Masache Kasaka aliyetaka kujua lini serikali itatoa maelekezo kwa ofisi ya mkuu wa Mbeya kufanya maombi maalum ya fedha kwaajili ya ujenzi wa Ofisi hiyo.

Akijibu swali hilo, Mhe. Dkt. Dugange amesema “Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeshawasiliana na mkuu wa mkoa wa Mbeya na kumpa maelekezo kupitia katibu Tawala wa mkoa kuleta bajeti kwaajili ya ujenzi wa Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chunya nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI kusisitiza maelekezo hayo kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya ili wakati wa bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2025/26 walete maombi hayo.”

Mhe. Dkt. Dugange amesema Serikali imeandaa michoro na gharama za ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya ambapo kiasi cha Sh.Bilioni 3.5. kinahitajika.

“Kwa kuwa kipindi cha maandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2025/26 kimefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya itawasilisha maombi hayo katika mpango na bajeti Mkuu wa Wilaya ya Chunya,” amesisitiza.

Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya lililopo kwa sasa lilijengwa mwaka 1937 na sasa jengo hilo ni chakavu na kumekuwapo na juhudi za ukarabati kufanyika mara kwa mara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news