Ujenzi wa Uwanja Arusha wafikia asilimia 25

ARUSHA-Kabla ya ujenzi wa uwanja huo mpya utakaoitwa Dr. Samia Suluhu Hassan, Arusha walikuwa na uwanja mmoja unaomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Sheikh Amri Abeid ambao ni wa zamani na umekuwa ukitumiwa kwenye michezo mbalimbali ya soka.
Dondoo muhimu kuhusu uwanja huo.

1. Uwanja unajengwa katika eneo la Mirongoine, Kata ya Olmoti ndani ya Jiji la Arusha.

2. Ujenzi utafanyika kwa muda wa miezi 24.

3. Utakuwa kati ya viwanja bora vya mpira Barani Afrika.

4. Utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000

5. Unajengwa kwa mchanganyiko wa muonekano wa madini ya Tanzanite, Mlima Kilimanjaro, Eneo la Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti.

6. Unajengwa sambamba na viwanja viwili vya mazoezi na baadaye utaendelezwa kwa kujengwa Bwawa la Kuogelea, viwanja Tenisi, Baskketball na Hosteli.

7. Utawekwa vyumba maalum vya watu mashuhuli (Directors Boxes).

8. Utatumika katika Fainali za AFCON 2027.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news