DODOMA-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatarajiwa kutia saini Mkataba wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu jijini Dodoma Februari 13, 2025 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uwanja huo.

Aidha,uwanja huo utakua na uwezo wa kubeba watu 32,000 kwa wakati mmoja.