Ukata waikabili timu ya Taifa ya Ngumi ya Wanawake

DAR-Shirikisho la ngumi Tanzania BFF linahitaji jumla ya shilingi 166,099,710 kufanikisha kwa mafanikio ushiriki wa timu ya Taifa ya ngumi katika mashindano ya ubingwa wa Dunia kwa wanawake.
Mashindano hayo yanategemewa kufanyika nchini Serbia katika mji wa Nis kuanzia Machi 6 hadi 17, mwaka huu.

Pesa hizo zinazohitajika zitakamilisha gharama zote za kambi wakati wa mazoezi ya maandalizi pamoja na kukamilisha malipo ya safari ikiwa ni tiketi za ndege chakula na malazi wakiwa nchini Serbia, bima pamoja na posho.

Leo timu hiyo imeanza mazoezi rasmi katika chuo cha taaluma ya Polisi DPA kilichopo kurasini jijini Dar es salaam ikiwa na jumla ya mabondia 16 na makocha watatu baada ya kuongezwa katika kikosi hiko bondia Martha Patrick kutoka timu ya NGOME.

Kufanikiwa kushiriki kwa mashindano hayo italeta tija kwa maendeleo ya michezo Tanzania na kwa mabondia wanawake watakaoshiriki kwani kuna uwezekano wa kujikomboa kiuchumi hasa kutokana na zawadi watakazopata washindi wa mashindano hayo kwa jumla ya USD 2.88 milioni zilizoandaliwa kwa ujumla kwa mgawanyo kama ifuatavyo.

Medali ya dhahabu zawadi yake USD 100, 000 sawa na milioni 255 za kitanzania.

Medali ya fedha USD 50,000 sawa na milioni 126. 9na laki tano za kitanzania.

Medali ya shaba USD 25,000 sawa na milioni 63. 5 za kitanzania.

Tano bora USD 10,000 sawa na milioni 25. 4 za kitanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news