
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdul-Razaq BADRU, akiongea na Waandishi wa Habari baada ya uzinduzi wa Mfumo wa Vikao vya Baraza hilo, pasipo kutumia Karatasi (PSSSF paperless Baraza Meeting Proceedings) katika hoteli Regency & Resort, kandokando mwa Ziwa Singidani, katika Manispaa ya Singida, leo Februari 6, 2025). Sambamba na hilo, Bw. Badru leo ametimiza miezi 12 ya utumishi katika Mfuko wa PSSSF na ameainisha mambo 12 kuelezea uongozi wake katika taasisi hiyo. Bw. Badru ametoa shukran nyingi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyemteua, Wizara - Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana, na Wenye Ulemavu), Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Mfuko huo.
Mfumo wa kutotumia karatasi katika nyaraka za vikao, utakaosaidia kupunguza gharama, muda wa kuandaa makabrasha, na kusaidia kuongeza ufanisi zaidi, umezinduliwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PSSSF, Bi. Joyce Mapunjo.