SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo ya vijijini kwa kufikisha umeme katika maeneo muhimu ya kijamii.
Baada ya kufikisha umeme kwenye vituo vya kuzalisha maji (pampu za maji) wananchi wanaeleza bayana namna ambavyo maisha yao yamebadilika kulinganisha na hali ilivyokuwa hapo kabla...