Wajasiriamali Comoro washauriwa kutumia usafiri wa anga

MORONI-Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Saidi Yakubu amewataka wajasiriamali wa nchi hiyo kufikiria kutumia usafiri wa anga kusafirisha bidhaa zao kutoka Tanzania na kuondokana na dhana kuwa usafiri huo ni ghari.Ameyasema hayo alipofanya kikao nao Februari 14, 2025 kujadili namna ya kupata ufumbuzi wa changamoto wanazokutana nazo katika biashara zao hasa usafirishaji wa bidhaa.

"Sambamba na usafiri wa majini ni vyema pia mkaanza kutumia usafiri wa anga kwa kuwa mashirika ya ndege ya Tanzania yako tayari kuwasikiliza na kuwapa bei nzuri na hivyo kuwawezesha kuleta bidhaa zenu kwa haraka zaidi,"Balozi Yakubu alisema.
Katika kikao hicho, wafanyabiashara hao walielezea changamoto kadhaa wanazokumbana nazo katika viwanja vya ndege na kuomba Ubalozi uzifikishe kwa mamlaka husika ili ziweze kufanyiwa kazi.

Biashara baina ya Comoro na Tanzania imekuwa ikiongezeka katika miaka ya hivi karibuni hususan katika bidhaa za chakula, nguo na vifaa vya ujenzi.
Katika kikao hicho, Balozi Yakubu aliambatana na Maafisa wa Ubalozi, Bw. Salim Haji na Bi Lilian Kimaro ambao wote kwa pamoja waliahidi kushirikiana na wajasiriamali hao ili kuendelea kukuza biashara kati ya Tanzania na Comoro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news