Wajifunza shughuli za usimamizi wa vyombo vya baharini Zanzibar

ZANZIBAR-Watendaji wa Taasisi ya Kikanda ya Mashariki, Kusini na Kaskazini mwa Afirika wamefanya ziara Maalum ya kujifunza Shughuli za Usimamizi wa Vyombo vya Baharini katika Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA).
Akiwakaribisha wageni wake kwenye Ofisi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini ( ZMA) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mtumwa Said Sandal amesema Zanzibar kupitia ZMA imekua kituo cha Mafanikio makubwa kwa Shughuliza za usimamizi wa Usafiri Baharini kwenye Kanda ya Afrika ndio maana Wageni hao wakafika Kujifunza kazi zinavyosimamiwa na Mamlaka.

Aidha,Mkurugenzi Sandal amewashukuru wageni hao kutoka Nairobi kwa kuona haja ya kufika Zanzibar na kujifunza shughuli za usimamizi wa vyombo vya Baharini na usalama wa abiria.

Akiwafundisha wageni hao juu ya Namna ya Usajili na Usimamizi wa Meli za Ndani na za Kimataifa Mohammed Nyona Haji kutoka Kitengo cha Usajili wa Meli na Mabaharia ZMA. Amesema Zoezi la Usajili limekuwa moja ya Mafanikio Makubwa kwa Mamlaka ya Usafiri Baharini ZMA na Taasisi nyingi za Ndani na za Kimataifa wamekua wakifika Zanzibar kwa Nyakati tofauti Kujifunza.

Aidha, Bwana Nyona amesema ujio wa Teknologia ya Habari na Mawasiliano umesaidia sana kuongeza mafanikio kwa Mamlaka na Taasisi za Kikanda na Kimataifa wanaofanya kazi za Usajili wa Meli. Amesema kwa sasa Mamalaka inaendelea kutumia Mifumo ya kisasa ili kuwasiliana na wenzao walio nje ya Zanzibar katika usajili wa Meli.

Nao wageni kutoka Taasisi ya Masula ya Udhibiti wa Shughuli za Baharini kutoka Kanda ya Mashariki, Kusini na Kaskazini mwa Afrika Bwana Aderick Kagenzi na Jonah Mumbya wamesema hakutegemea kukuta mambo makubwa na mazuri yanayofanyika kwenye Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA ) hasa kwenye hili eneo la Usajili wa Meli na kwamba wamechukua ujumbe mzito kwenda kuuwasilisha katika Taasisi yao kuhusiana na Mafanikio ya ZMA.

Kwa upande wake Ndugu Jonah Mumbya amesema zipo fursa nyingi kwa Taasisi za Usimamizi wa Shughuli za Baharini na Usajili wa Meli kwamba Mamlaka ya Usafiri Baharini isisite kufanya kazi kwa Karibu na taasisi hiyo.

Wageni hao kutoka Taasisi ya Usafiri Baharini kutoka Kanda ya Mashariki, Kusini na Kaskazini mwa Afrika wamekamilisha ziara yao ya siku moja hapa Zanzibar

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news