Wakandarasi wasimamiwe kutekeleza miradi ya nishati kwa wakati-Kapinga

TANGA-Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amewataka watendaji wa Sekta ya Nishati kuwajengea uwezo watoa huduma wanaotekeleza miradi mbalimbali ya sekta ya nishati nchini.
Hayo ameyasema leo Februari 23, 2025 na Kapinga wakati akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO, na wakuu wa taasisi za wizara kabla ya kushiriki ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan inayotarajiwa kuanza leo mkoani Tanga.

"Tunataka hii miradi ikamilike kwa wakati na kwa ubora mkubwa, wakandarasi wajengewe uwezo wa utendaji kazi ili kazi ionekane inafanyika,"ameongeza Mhe. Kapinga.
Aidha, ameipongeza REA kwa kumaliza kufikisha umeme kwenye vijiji vyote nchini na kusisitiza miradi inayoendelea na ile inatakayoanza mwaka huu wa fedha itekelezwe kwa wakati.

"Ni muhimu sana kuwasimamia wakandarasi kwa nguvu kuanzia mwanzo tuwe nao makini ili miradi hii ya kupeleka umeme kwenye vitongoji ikamilike kwa wakati,"amesema Mhe. Kapinga.
Katika hatua nyingine, Mhe. Kapinga amewataka watendaji wa taasisi za nishati kuwa na mahusiano mazuri na wananchi hususan wakati wa kupitisha miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.

"Imarisheni mahusiano na wananchi mnapopitisha miradi yetu na kuwaeleza kuwa Serikali italipa fidia kwa wote miradi hiyo ilipopita,"amesema Mhe. Kapinga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news