Wanafunzi wajiteka Dar wapate fedha kwa wazazi

DAR-Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia wasichana wawili kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na watekaji kudai pesa kutoka kwa familia zao pesa.
Akizungumza Februari 04, 2024, Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Januari 26, 2025 baada ya kutolewa taarifa za kupotea kwa mabinti hao Jeshi lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwapata na kisha kuwahoji kwa kina juu ya tukio hilo wasichana hao wawili ambao ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili (16) na mwingine Mwanafunzi wa Darasa la saba (12) wakazi wa Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kamanda muliro alisema wasichana hao wanashikiliwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira ambayo yanaonyeshe kuwa wametekwa na watekaji wanataka pesa.

“Katika uchunguzi wetu na ufuatiliaji ulifaonywa na jeshi la polisi mara baada ya mahojiano ya kina na watoto hao ambao walikiri kutengeneza tukio hilo la uongo ili waweze kujipatia pesa kwa udanganyifu toka kwa wazazi wao."

Alisema mara baada ya kutoweka Januari 26, 2025 na kuelekea Longoni Beach ambapo walikesha hapo hadi Januari 27 asubuhi na baadae kuelekea maeneo ya Tungi mpaka walipokamatwa wakiwa wakizunguka.

“Jeshi linalaani na kukemea vikali vitendo hivyo vya watu kujiteka kwa lengo la kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu na kusisita kuwa jeshi alitasita kuwachukua hatua kali wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news