Wananchi washauriwa kujisajili Wezesha Portal

NA EVA NGOWI
WF Kilimanjaro

SERIKALI imewashauri wananchi kusajili vikundi vyao vya huduma ndogo za fedha kupitia mfumo wa Wezesha Portal ambayo ni njia rahisi na haina gharama yoyote.
Baadhi ya Wanavikundi na Wajasiriamali wadogo wadogo wakisikiliza elimu ya fedha, uwekezaji na utaratibu wa kujiunga na vikundi iliyofanyika katika Kata ya Kibosho, Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.

Ushauri huo umetolewa na, Afisa Usimamizi Fedha Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Jackson Mshumba wakati akitoa Elimu ya Huduma Ndogo za Fedha katika Kata ya Kibosho, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoani Kilimanjaro.
Afisa Usimamizi Fedha Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Jackson Mshumba, akitoa elimu ya usajili wa vikundi vya huduma ndogo za fedha katika Kata ya Kibosho, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa Wezesha Portal ni jukwaa la dijitali lililoundwa kusaidia wajasiriamali na wafanyabiashara katika kukuza biashara zao, kupata mafunzo, na kupata rasilimali zingine za kuwasaidia kibiashara na inaokoa muda.

Aidha, Bw. Mshumba alisema kuwa kabla ya kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha ni vyema wananchi wanaotaka kuanzisha vikundi hivyo wakajiridhisha kuhusu wanachama wao wanaotaka kujiunga nao ili kuepukana na lawama na baadhi ya wajumbe kukimbia familia zao kutokana na madeni.
Afisa Usimamizi Fedha Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Jackson Mshumba, akitoa elimu ya fedha, utaratibu wa kujiunga na vikundi kwa Kata ya Kibosho, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoani Kilimanjaro.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Kilimanjaro).

“Kabla ya kujiunga kwenye kikundi kitu cha kwanza lazima wawe wanatoka eneo moja ili kurahisisha utambuzi katika Serikali za Mitaa, pili, lazima waaminiane, tatu, wawe na lengo moja lililosababisha wao waamue kuanzisha kikundi,"alisema Bw. Mshumba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news