Wanne mahakamani kwa kuongoza genge la uhalifu Dar

DAR-Watu wanne wamepandisha kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka 49 yakiwemo kuongeza genge la uhalifu na utakatishaji fedha kiasi cha shilingi 5,000,000 walizojipatia kwa njia za udanganyifu.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Eradius Rwechungura (43) maarufu ‘Rwamakala’, Heri Kabaju (37) maarufu ‘Babylon’, Abdurahim Karugila (42) maarufu 'Obra' na Eradius Apornary(22) walidaiwa kujiwasilisha kuwa ni maofisa kutoka sehemu mbalimbali na kujipatia fedha huku wakijua si kweli.
Washitakiwa walifikishwa Mahakamani hapo jana jioni Januari 31, 2025 na kusomewa mashitaka yao yanayowakabili na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nura Manja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Akisoma hati ya mashitaka wakili Manja alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 49, moja likiwa ni la Kuongoza genge la uhalifu, 11 ya kujiwasilisha kwa utambulisho wa mtu mwingine, 13 ya kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine na, 23 ya kujipatia fedha kwa njia za udangifu na moja la utakatishaji fedha.

Wakili Manja alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo aliiomba Mahakama ipange tarehe nyingine ya kesi kutajwa.

Washitakiwa walirudishwa ramande na shauri hilo liliahirishwa hadi Februari 14, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news