ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema,wasanii wana mchango muhimu wa kuhamasisha jamii kushiriki matukio muhimu ya kijamii kwa ufanisi na kuleta mabadiliko chanya.

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Msanii wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva) Mbwana Yussuf Kilungi (Mbosso) aliyefika Ikulu Zanzibar tarehe 17 Februari 2025.
Aidha, Dkt. Mwinyi amempongeza kwa hatua ya Msanii kuamua Kuunga mkono juhudi za Serikali kwa hiyari na kuahidi ushirikiano wa kutosha kufanikisha dhamira yake.
Rais Dkt.Mwinyi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuwa karibu na wasanii katika matukio mbalimbali.
Naye Msanii Mbosso ameeleza kuridhishwa na juhudi za Rais Dkt, Mwinyi za kuleta Maendeleo Zanzibar na kuahidi kutumia kipaji chake kuyatangaza Maendeleo yanayofanyika hivi sasa.