MWANZA-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amemjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu yaTaifa (NEC), ndugu Christopher Gachuma ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Bugando jijini Mwanza.

Majeruhi mwengine katika ajali hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, ndugu Kemilembe Ruta pamoja na dereva wa gari hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya hospitali hiyo, majeruhi wote wa ajali hiyo wanaendelea vizuri.