Watumishi Ofisi ya Rais-Utumishi wahimizwa kubadili mfumo wa maisha ili kujiepusha na maradhi yasiyoambukiza

NA VERONICA MWAFISI

WATUMISHI wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wametakiwa kuzingatia na kubadili mfumo wa maisha ili kujiepusha na maradhi yasiyoambukiza kwa lengo la kuwahudumia wananchi pasipokuwa na changamoto zozote za kiafya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge akifanya wasilisho kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa watumishi wa ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.

Wito huo umetolewa leo Februari 24, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge wakati akiwasilisha mada kuhusu afya kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Dkt. Kisenge amesema Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu yanatokana na namna watu wanavyoendesha maisha yao hivyo, ni vema kupunguza matumizi makubwa ya sukari na matumizi ya ulaji wa chumvi nyingi inayosababisha shinikizo la juu la damu ambalo moja ya madhara yake ni kutanuka kwa moyo ambao matibabu yake ni gharama kubwa.

Aidha, Dkt. Kisenge amewataka watumishi wa ofisi hiyo kujitahidi kutumia mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora ili kukabiliana na magonjwa ya moyo.

Dkt. Kisenge ametoa wito kwa watumishi hao kupima afya zao mara kwa mara ili kujua tatizo mapema pamoja na kupunguza gharama za matibabu kwani ugonjwa ukishakuwa mkubwa gharama huongezeka zaidi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo kuhusu utunzaji wa afya bora yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi yake.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo kuhusu utunzaji wa afya yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyesimama) akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa mafunzo kuhusu utunzaji wa afya bora yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (katikati) akifuatilia wasilisho kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa watumishi wa ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo kuhusu utunzaji wa afya bora yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo kuhusu utunzaji wa afya bora yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Stephano Mgala (aliyenyanyua mkono) akiuliza swali kuhusu afya mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge (hayupo pichani) kuwasilishwa mada kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu wakati wa mafunzo yanayotolewa kwa watumishi wa ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (wa kwanza kushoto) akifuatilia wasilisho kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu wakati wa mafunzo yanayotolewa kwa watumishi wa ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi. Wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge (hayupo pichani) wakati akifanya wasilisho kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu kwenye mafunzo yaliyofanyika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge (hayupo pichani) wakati akifanya wasilisho kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu kwenye mafunzo yaliyofanyika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.

Akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amemshukuru Dkt. Kisenge pamoja na wataalamu alioambatana nao kwa kutoa elimu hiyo kwa watumishi wa ofisi yake na kuahidi kuzingatia suala la afya ili kutoa huduma bora kwa wananchi kwa ustawi wa Taifa la Tanzania.

Mafunzo hayo ni mwendelezo wa utaratibu uliowekwa na Ofisi ya Rais –UTUMISHI wa kutoa uelewa kuhusu masuala mbalimbali katika Utumishi wa Umma ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news