Wazazi washauriwa kuwafundisha watoto umuhimu wa kuweka akiba

NA EVA NGOWI
WF Kilimanjaro

SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha imewashauri wazazi na walezi kuwafundisha Watoto kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba ili kuwasaidia katika Maisha yao ya baadae.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Salimu Kimaro, akitoa elimu ya fedha kuhusu Akiba na Bajeti kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwika iliyoko Kata ya Mwika Kaskazini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionensia Mjema, wakati wa semina zinazoendelea katika miji na vijiji mkoani Kilimanjaro, ikiwemo Shule za Sekondari, Mangi Mariale iliyopo Kata ya Mwika Kusini na Mwika Sekondari iliyopo Kata ya Mwika Kaskazini Wilaya ya Moshi Vijijini.

Bi. Mjema alisema kuwa kuwafundisha Watoto kuweka akiba kutawajengea mfumo madhubuti wa kujenga uhakika wa masuala ya kifedha.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionensia Mjema, akitoa Elimu ya Fedha kwa Wanafunzi walioshiriki semina ya Elimu ya Fedha kuhusu Umuhimu wa kuweka Akiba iliyofanyika katika Sekondari ya Mwika, Kata ya Mwika Kaskazini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.

“Watoto wengi wamekiri kwamba walikuwa hawafahamu kwamba wanapopewa pesa wanatakiwa watumie kiasi na kiasi kingine waweke kama akiba ili siku wazazi wao wanapokosa pesa za kuwapa waweze kuzitumia,”alisema Bi. Mjema.
Wanafunzi wa Sekondari ya Mwika wakisikiliza Elimu ya umuhimu wa kuweka Akiba kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Bi. Dionensia Mjema (hayumo pichani) iliyofanyika katika Sekondari ya Mwika, Kata ya Mwika Kaskazini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.

Bi. Mjema alisema kuwa kwa sasa kuna Taasisi mbalimbali kama vile Benki, Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS zinatoa elimu kwa Watoto kuhusu namna ya kuweka akiba, hivyo ni muhimu kwa wazazi na walezi kutumia fursa hizo kwa ajili ya Watoto wao.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Salimu Kimaro, akitoa elimu ya fedha kuhusu Akiba na Bajeti kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mangi Mariale iliyoko Kata ya Mwika Kusini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro

Awali, akifundisha wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mwika, Bi. Mjema aliwataka wanafunzi hao wawe na tabia ama utamaduni wa kupanga bajeti ili wapate akiba ya kuweka, kutoka katika fedha wanazopewa na wazazi kwa ajili ya matumizi yao ya kawaida na kununua vitu ili waweke akiba kiasi fulani cha fedha kinachobaki.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Mkuu kutoka Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi akiwapongeza wanafunzi waliojibu maswali vizuri baada ya kupata Elimu kutoka kwa Wataalamu wa Wizara ya Fedha katika Shule ya Sekondari ya Mareale iliyopo Kata ya Mwika Kusini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.
Picha ya Pamoja ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mareale mara baada ya kumaliza semina ya Elimu ya Fedha iliyofanyika katika shule hiyo iliyopo Kata ya Mwika Kusini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Kilimanjaro).

Vilevile Bi. Mjema alisema kuwa kuweka akiba ni njia za kuondokana na madeni yanayotokana na matumizi ya kila siku pamoja na gharama nyingine za maisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news